• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu 73 wafa kwenye mlipuko mkubwa Beirut

    (GMT+08:00) 2020-08-05 09:57:13

    Mlipuko mkubwa uliotokea jana jioni kwenye eneo la bandari mjini Beirut, Lebanon, mpaka sasa umesababisha vifo vya watu 73 na wengine 3,700 kujeruhiwa.

    Mlipuko huo umeharibu vibaya mitaa mingi mjini Beirut, wakazi kwenye mtaa wa Achrafieh karibu na eneo la mlipuko wamesema mtaa wote umeharibiwa kama umekumbwa na maafa na watu wengine wamejeruhiwa. Habari kutoka vyombo vya habari zinasema majengo ya ikulu ya Lebanon yaliyoko kilomita zaidi 10 mbali na mlipuko huo pia yameharibiwa.

    Baada ya mlipuko huo kutokea, magari mengi ya wagonjwa yameenda kusafirisha majeruhi na miili ya wahanga. Jeshi la Lebanon pia limetuma helikopta kusaidia kuzima moto. Jeshi la polisi pia limefunga maeneo yaliyo karibu na mlipuko huo na kuwazuia watu kuingia kwenye eneo la bandari.

    Hadi sasa chanzo cha mlipuko bado hakijajulikana, lakini waziri wa mambo ya ndani wa Lebanon Bw. Mohammad Fahmy, amesema huenda mlipuko huo umesababishwa na kemikali ya Ammonium nitrate iliyowekwa kwenye ghala la bandari kuanzia mwaka 2014.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako