• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Howe aishusha Bournemouth daraja kisha ang'atuka

  (GMT+08:00) 2020-08-05 15:41:26

  Bournemouth wameagana rasmi na kocha wao Eddie Howe baada ya kushushwa ngazi kwenye Ligi Kuu ya Uingereza (EPL). Miaka mitano ya Bournemouth katika EPL ilifikia tamati Julai 26 licha ya kuifunga Everton mabao 3-1 uwanjani Goodison Park. Sare ya 1-1 ya Aston Villa dhidi ya West Ham United uwanjani London ilihakikisha kwamba Bournemouth wanashuka ngazi kwa pamoja na Norwich City na Watford. Howe, 42, aliwaongoza Bournemouth katika jumla ya mechi 450 katika awamu mbili za ukocha chini ya miaka 10 iliyopita. Katika taarifa yake, Howe ambaye ni mzawa wa Uingereza alisema anaamini kwamba huu ni wakati mwafaka zaidi kwa klabu yake kupata mabadiliko.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako