• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Victor Osimhen mwanasoka ghali zaidi Ulaya Mwafrika

  (GMT+08:00) 2020-08-05 15:42:18

  Timu ya Napoli inayoshiriki Ligi Kuu ya Italia (Serie A) imemsajili mshambuliaji chipukizi mzawa wa Nigeria, Victor Osimhen kutoka Lille ya Ufaransa. Katika taarifa yao, Napoli wameekeza furaha yao kumsajili Osimhen kwa mkataba wa kudumu kutoka Lille. Uhamisho wa Osimhen unakadiriwa kugharimu Napoli kima cha Euro milioni 70, na kumfanya kuwa mwanasoka ghali zaidi kutoka barani Afrika. Osimhen alijiunga na Lille mwanzoni mwa msimu huu wa 2019-20 akichukua nafasi iliyoachwa wazi na Pepe baada ya kushawishiwa na Lille kuagana na Charleroi inayocheza Ligi Kuu ya Ubelgiji.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako