• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Ligi Kuu Tanzania kuanza Septemba 6

  (GMT+08:00) 2020-08-05 15:43:06

  Bodi ya Ligi Tanzania (TPBL) jana imetangaza rasmi tarehe ya kuanza kwa msimu mpya wa ligi mbalimbali, ambapo Ligi Kuu Tanzania Bara itaanza Septemba 6 mwaka huu. Bodi hiyo pia imesema, Ligi Daraja la Kwanza (FDL) inatarajiwa kuanza Oktoba 3, huku Ligi Daraja la Pili (SDL) ikipangwa kuanza Novemba 7 mwaka huu. Taarifa iliyotolewa na Bodi hiyo imeeleza kuwa Ligi Kuu inatarajiwa kumalizika Mei 16 mwakani, huku FDL ikimalizika Mei Mosi mwakani, na SDL yenyewe itamalizika April 17 mwaka ujao. Lakini uongozi wa Bodi hiyo umesema ratiba hiyo inaweza kubadilika kutokana na kutangazwa kwa kalenda ya matukio ya ratiba ya FIFA, CAF na CECAFA.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako