• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sudan yakataa pendekezo la Ethiopia la kujaza na kutumia Bwawa la GERD

    (GMT+08:00) 2020-08-05 17:11:29

    Wizara ya Rasilimali Maji na Umwagiliaji ya Sudan imesema, nchi hiyo imekataa pendekezo la Ethiopia kuhusu kujaza na kutumia Bwawa la GERD.

    Taarifa iliyotolewa na Wizara hiyo imesema, Sudan imekataa pendekezo la Ethiopia kwa kuwa linaelekeza kuwa, makubaliano yanapaswa kuhusisha awamu ya kwanza tu ya kujaza Bwawa hilo, huku ikiunganisha makubaliano hayo na kufikia mkataba wa kina kuhusu maji ya Blue Nile.

    Kutokana na taarifa hiyo, Sudan inachukulia pendekezo hilo kama kubadilika kwa msimamo wa Ethiopia, ambao unatishia mwendelezo wa mazungumzo ya pande tatu kati ya Sudan, Misri na Ethiopia.

    Masharti ya awali ya Sudan kushiriki katika mazungumzo ya bwawa la Mto Nile ni kwamba makubaliano ya kujaza na kutumia bwawa la GERD hayapaswi kuunganishwa na kufikia mkataba kuhusu maji ya Blue Nile.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako