• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Baadhi ya Wamarekani wanasema hatua za kukabiliana na COVID-19 nchini Marekani si nzuri kama nchi nyingine

  (GMT+08:00) 2020-08-05 18:45:38

  Uchunguzi wa maoni ya raia uliofanyika kwa pamoja na shirika la NPR nchini Marekani na kundi la Ipsos umeonesha kuwa, karibu theluthi mbili ya wamarekani wameona kuwa hatua zilizochukuliwa na serikali ya nchi hiyo kukabiliana na COVID-19 nchini humo si nzuri kama nchi nyingine.

  Kutokana na uchunguzi huo, asilimia 41 ya wamarekani wameona kuwa hali ya kukabiliana na janga hilo nchini Marekani ni mbaya sana kuliko nchi nyingine, na asilimia 25 wameona hali hiyo nchini humo ni mbaya kidogo kuliko nchi nyingine, na watu wasiozidi theluthi moja wameona kuwa Marekani imekabiliana na janga hilo vizuri kuliko nchi nyingine.

  Mtaalamu wa uchunguzi wa maoni ya raia wa kundi la Ipsos amesema, kwa upande wa idadi ya vifo kutokana na maambukizi ya COVID-19 na ueneaji wa virusi hivyo, Marekani iko kwenye hali mbaya, na wamarekani wanataka kuona hatua zenye ufanisi zaidi za kupambana na janga hilo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako