• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sudani Kusini : Benki ya Dunia yaipa Sudani Kusini ruzuku ya dola milioni 40

    (GMT+08:00) 2020-08-05 18:46:17

    Benki ya Dunia imeidhinisha kibali ruzuku ya dola milioni 40 kusaidia Sudani Kusini kuboresha miundombinu ya msingi na kuimarisha taasisi za jamii.

    Fedha hizo zitafaidi raia 630,000 ambao wanaishi katika kaunti 21 kwa kuwezesha uwekezaji kwenye miundombinu ya jamii na huduma za jamii zinazopewa kipaumbele.

    Meneja wa Benki ya Dunia nchini Sudani Kusini Husam Abudagga alisema katika taarifa kuwa Sudani Kusini inapitia kipindi kikuu cha mabadiliko na kwamba fedha hizo zitasaidia watu kufikia huduma kwa urahisi na usawa.

    Mradi huo utatekelezwa na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Huduma, kwa kushirikiana na serikali na washirika wengine wa maendeleo.

    Waziri wa Fedha na Mipango wa Sudani Kusini Salvatore Garang Mabiordit alibaini kuwa serikali inaendelea kupokea misaada kusaidia hasa maeneo yaliyo hatarini ambayo yanakabiliwa na athari za mizozo ya vita, wakimbizi wanaorejea nyumbani na hatari za asili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako