• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Nigeria: Shirika la ndege la Air Peace Air Peace lapunguza wafanyakazi

  (GMT+08:00) 2020-08-05 18:47:19
  Shirika la ndege la Air Peace la Nigeria limetangaza kufuta idadi isiyojulikana ya marubani na kupunguza mishahara ya wafanyikazi kutokana na athari za janga la corona.

  Taarifa iliyotolewa na shirika jilo inasema uamuzi huo umechukuliwa kwa manufaa ya kampuni na maelfu ya wafanyikazi wakiwemo marubani walioathiriwa.

  Vyanzo vya habari nchini humo hata hivyo vinaripoti kuwa karibu marubani 70 wameathiriwa na upunguzwa kwa mishahara, ni kati ya asilimia 0 hadi 40 kulingana na daraja la mishahara ya wafanyikazi.

  Air Peace inahudumu katika miji mikubwa nchini Nigeria, Afrika Magharibi na Mashariki ya Kati.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako