• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Ethiopia: Ethio Telcom yapata dola bilioni 1.3 ndani ya mwaka mmoja

  (GMT+08:00) 2020-08-05 18:47:54
  Kampuni ya pekee ya rununu ya Ethiopia imetangaza kuwa imepata dola bilioni 1.3 katika kipindi kilichokamilika Juni 30, 2020.

  Kulingana na ripoti ya utendaji ya Ethiotelcom, mapato ya mwaka huu yaliongezeka kwa asilimia 105.1 ikiwa ni zaidi ya malengo ya kampuni hiyo kwa kipindi cha kati ya Julai 2019 na Juni mwaka 2020.

  Hilo ni ongezeko la asilimia 31.4 ikilinganishwa na mwaka uliopita.

  Kulingana na ripoti hiyo, dola milioni 147.7 ni kutoka kwa huduma za kimataifa.

  Idadi ya wateja wa Ethio Telecom imefikia milioni 46.2, ongezeko la asilimia 5.8 kutoka takwimu za mwaka jana.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako