• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yapinga ziara ya waziri wa afya wa Marekani mjini Taiwan

  (GMT+08:00) 2020-08-05 19:15:32

  Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Wang Wenbin leo hapa Beijing amesema, China inapinga imara mawasliano ya kiserikali kati ya Marekani na Taiwan.

  Kauli hiyo imekuja baada ya taarifa kuwa waziri wa afya wa Marekani Alex Azar hivi karibuni ataongoza ujumbe na kufanya ziara kwenye Taiwan.

  Bw. Wang amesema msimamo wa China ni wazi, na kanuni ya kuwepo kwa China moja tu ni msingi wa kisiasa wa uhusiano kati ya China na Marekani. Amesema China inaihimiza Marekani kufuata kanuni hiyo na taarifa tatu za pamoja kati ya China na Marekani, kusitisha mawasiliano yote ya kiserikali kati yake na Taiwan, na kushughulikia kwa makini masuala yanayohusu Taiwan, ili kutoharibu uhusiano kati ya China na Marekani na utulivu na amani ya eneo la bahari ya Taiwan.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako