• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais wa China atuma salamu za pole kwa rais wa Lebanon kutokana na mlipuko mkubwa uliotokea nchini humo

  (GMT+08:00) 2020-08-05 19:27:51

  Rais Xi Jinping wa China ametuma salamu za pole kwa mwenzake wa Lebanon Bw. Michel Aoun kutokana na mlipuko mkubwa uliotokea kwenye mji mkuu wa nchi hiyo, Beirut.

  Kwenye salamu hizo, rais Xi ameeleza kushtushwa na taarifa za mlipuko huo uliosababisha vifo na majeruhi ya watu wengi. Kwa niaba ya serikali na wananchi wa China, rais Xi ametuma salamu za rambirambi kwa familia za watu waliopoteza maisha, na kuwatakia majeruhi wapone mapema.

  Mlipuko mkubwa ulitokea jana jioni kwenye eneo la bandari mjini Beirut, Lebanon, na mpaka sasa umesababisha vifo vya watu zaidi ya 100 na wengine zaidi ya 4000 kujeruhiwa.

  Mlipuko huo umeharibu vibaya mitaa mingi mjini Beirut, wakazi kwenye mtaa wa Achrafieh karibu na eneo la mlipuko wamesema mtaa wote umeharibiwa na watu wengi wamejeruhiwa.

  Vyombo vya habari zinasema majengo ya ikulu ya Lebanon yaliyoko kilomita zaidi 10 mbali na mlipuko huo pia yameharibiwa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako