• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mwanariadha mkimbizi wa Sudan Kusini atangazwa kuwa balozi mwema wa UNHCR

  (GMT+08:00) 2020-08-05 20:10:47

  Mwanariadha mkimbizi wa Sudan Kusini ametangazwa kuwa balozi mwema wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataofa, UNHCR, kwa lengo la kutetea haki za wakimbizi.

  Yiech Pur Biel, ambaye alikimbia mapigano nchini Sudan Kusini mwaka 2005 na kuishi kwenye kambi ya wakimbizi ya Kakuma nchini Kenya akiwa na umri wa miaka 10, ametajwa kuwa balozi wa hiari wa UNHCR ili kuendelea kutetea haki za watu waliopoteza makazi yao wakati akiendelea na mazoezi yake ya kushiriki katika Mashindano ya Olimpiki ya Wakimbizi yatakayofanyika Tokyo mwaka 2021.

  Pur amesema, ni heshima kubwa kwake kuweza kutumia nafasi yake kama mwanariadha kusaidia wakimbizi na watu waliokimbia makazi yao, kusimulia historia yake na wakimbizi wengine kama yeye, na kuhakikisha kuwa wakimbizi duniani kote wanapaza sauti yao.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako