• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda:Mfumo mpya wa kielektroniki wa mnada utazuia rushwa

    (GMT+08:00) 2020-08-06 18:41:17

    Katika juhudi za kupambana na rushwa katika mchakato wa kupiga mnada mali za waliochukuwa mikopo,serikali ya Rwanda jana ilizindua mfumo mpya wa kielektroniki ambao utapunguza rushwa katika mchakato huo.

    Mfumo huo unalenga kupunguza ushiriki wa watu katika mchakato wa mnada ,na hivyo kupunguza rushwa na mali kuwekwa thamani ya chini.

    Msajili Mkuu Richard Kayibanda alisema kuwa mfumo huo utawawezesha walio na nia ya kushiriki mnada kufanya hivyo wakiwa sehemu yoyote ile,iwe ni Rwanda au nje ya nchi kwa sababu mnada utafanywa mtandaoni.

    Alisema kuwa matumizi ya mfumo huo utafanya mchakato uwe wazi zaidi na kufanya mazingira yam nada kuwa rafiki kuliko awali ambapo madalali waliwahujumu walioshiriki mnada.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako