• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania yatuzwa

    (GMT+08:00) 2020-08-06 18:41:48
    Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imepewa tuzo kutokana na kutambua mchango wa mikopo yake ambayo imetoa ili kuimarisha ushirika nchini.

    Kwa kipindi cha mwaka mmoja benki hiyo imeshatoa zaidi ya Sh. bilioni 100.

    Akitoa tuzo hiyo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Angellah Kairuki, aliisifu benki hiyo na kusema vyama vya ushirika vikuu na vya msingi vimepata wadau imara na wanaotatua matatizo ambayo siku za nyuma yalikuwa yakikwamisha ushirika nchini.

    Kwa upande wake,Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina ameisifu Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) kwa jitihada za kuchochea uongezekaji wa tija katika uzalishaji na mapato ya Watanzania wanaojiajiri katika sekta za mifugo na uvuvi.

    Waziri Mpina alisema kuwa TADB imekuwa mstari wa mbele katika kushirikiana na mabenki washirika kuwakopesha wadau wa sekta ya uvuvi na ufugaji na kwa hiyo kuzifanya sekta hizo ziwe na maana kwa Watanzania.

    Aidha ameisifu benki hiyo kwa kuongeza mnyororo wa thamani kwa bidhaa zinazotokana na uvuvi na ufugaji kwa kufufua viwanda vikubwa vya maziwa, kikiwemo kiwanda cha maziwa cha ushirika mkoani Njombe.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako