• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya:Mamlaka ya Mapato yatoa makataa kwa waliochelewa kulipa ushuru

  (GMT+08:00) 2020-08-06 18:42:08
  Watu binafsi na biashara nchini Kenya wana hadi mwisho wa mwezi huu kutuma maombi ya kusamehewa kodi au mali zao zishikwe ama kupigwa mnada.

  Mamlaka ya Mapato Nchini Kenya (KRA) imesema inadai takriban Sh250 bilioni katika malimbikizi ya ushuru.

  Mamlaka hiyo aidha imesema kuwa wanaoidaiwa wana hadi tarehe 30 Agosti kutuma maombi ya kusamehewa malimbikizi ya riba na adhabu ya kutolipa ushuru kwa wakati.

  Chini ya sheria ya kusamehewa malimbikizi ya riba ,watu binafsi na biashara wanafaa kutoa ushahidi unaoonyesha kuwa wanapitia hali ngumu za kifedha na hawawezi kulipa adhabu au riba ambazo KRA imewapatia kwa kutolpia kodi kwa wakati.

  Katika ilani iliyotolewa na Kamishna wa Kodi za ndani wa KRA,Elizabeth Meyo,mamlaka hiyo inasema kuwa imemaliza mchakato wa uboreshaji mfumo kwa ajili ya uchakataji wa maombi ya kusamehewa adhabu za kutolipa kodi kwa wakati.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako