• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wataalamu wa nchi mbalimbali wasema kurudisha ushirikiano kati ya China na Marekani kunaendana na maslahi ya pamoja kati yao

    (GMT+08:00) 2020-08-07 17:07:16

    Wataalamu wa nchi mbalimbali wamesema, uhusiano kati ya China na Marekani ni uhusiano muhimu wa pande mbili duniani, na kutatua mzozo kwa njia ipasavyona kurudisha ushirikiano kati ya nchi hizo kunaendana na maslahi ya pamoja kati ya pande hizo mbili na jumuiya ya kimataifa.

    Mjumbe wa taifa wa China ambaye pia ni waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi hivi karibuni alisema, China inataka kukabiliana na msukumo kwa utulivu na kutuliza hali ya wasiwasi kupitia mazungumzo ya usawa na ya kiujenzi.

    Mkurugenzi wa kituo cha utafiti wa mambo ya China katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Tanzania Bw. Humphrey Moshi amesema, katika miaka mingi iliyopita mawasiliano kati ya China na Marekani yalihimiza amani na utulivu wa dunia na maendeleo ya uchumi na jamii, na sera ya "vita mpya ya baridi" si mpango wa kutatua mgogoro, bali mazungumzo ni njia yenye ufanisi ya kutatua suala.

    Mtaalamu wa masuala ya kimataifa pia amesema hivi sasa dunia inakabiliana na changamoto mbalimbali, ambazo zinahitaji mfumo wenye nguvu na ufanisi mkubwa zaidi wa pande nyingi wa ushirikiano. China na Marekani zikiwa makundi mawili makubwa zaidi duniani, zinahitaji kurejesha uhusiano kati yao kwenye hali ya kawaida mapema, na kutatua migogoro kati yao kwa njia ya kuaminiana na kuheshimiana.

    Mchunguzi wa taasisi ya Schiller ya Ufaransa Bibi Christine Bière amesema, Ufaransa na nchi nyingine za Ulaya zinapinga vita mpya ya baridi, na hazitaki kuharibu zaidi uhusiano kati ya China na Marekani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako