• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tanzania: Wakulima wa kawaha walia bei kuwa ndogo

  (GMT+08:00) 2020-08-10 17:47:41

  Wakulima wa kahawa nchini wamelalamikia kupata hasara kila msimu wa mauzo kutokana na bei ndogo wanayoipata, jambo ambalo haliendani na gharama halisi za uzalishaji wa kahawa.

  Wakizungumza kwa nyakati tofauti wikendi iliyopita katika shamba, darasa la Taasisi ya Utafiti wa Kahawa Nchini (TaCRI), lililopo katika maonyesho ya wakulima ya nanenane Kanda ya kaskazini, viwanja vya Themi Arusha, baadhi ya wakulima hao walisema bei ya zao hilo inazidi kuwadidimiza wakulima.

  Baadhi wanasema kwa wamekuwa wakipata hasara ambapo gharama za uzalishaji wa kahawa kwa kilo moja ni Sh 4,500 huku Bei wanayoipata sokoni kiwa ni Sh 3,900. Mbali na changamoto ya bei ya zao hilo kuwa chini, wanakabiliwa na ukosefu wa pembejeo jambo ambalo limekuwa likisababisha kuongeza gharama katika uzalishaji.

  Kwa upande wake Mtafiti kutoka TaCRI, Sophia Malinga, amekiri kuwepo kwa changamoto nyingi zinazo wakabili wakulima ikiwemo ukosefu wa maji ya kutosha ya umwagiliaji wa bustani za miche katika halmashauri zote nchini.

  Akizungumzia suala la bei ya kahawa, Meneja wa Mauzo na Ubora kutoka Bodi ya Kahawa nchini (TCB), Frank Nyarusu, alisema msimu kwa sasa wameruhusu wanunuzi binafsi kununua kahawa kwa wakulima kupitia vyama vya ushirika jambo ambalo litasaidia kuondoa ukandamizaji kwa wakulima.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako