• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tanzania: TRA yaja na mfumo wa kuwasilisha ritani kielektroniki

  (GMT+08:00) 2020-08-10 17:48:07

  Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imeanzisha mfumo wa uwasilishaji ritani za kodi kwa njia ya kielektroniki (e-Filing System) ukiwa na lengo kurahisisha uwasilishaji wa ritani za kodi na kupunguza gharama kwa upande wa mlipakodi.

  Akizindua mfumo huo jijini Arusha, Kamishna Mkuu wa TRA Dk. Edwin Mhede, alisema mfumo huo mpya utaongeza tija katika usimamizi wa kodi na kuboresha uwasilishaji wa ritani ambapo mlipakodi ataweza kuwasilisha ritani za kodi na kupata hati ya madai kwa ajili ya kufanya malipo bila kutembelea ofisi za TRA.

  Mfumo huu pia unamwezesha mlipakodi kujua taarifa za ritani za kodi zinazotakiwa kuwasilishwa kwa kipindi husika na hivyo kuziwasilisha ndani ya muda stahiki na kuepuka faini ya kuchelewa kuwasilisha ritani hizo.

  Dk Mhede alisema mfumo huo umetengenezwa katika namna ambayo unakumbusha mlipakodi tarehe ya mwisho ya kuwasilisha ritani na kulipa kodi zake stahiki na hivyo kupunguza uwezekano wa kutozwa riba na adhabu zinazotokana na kuchelewa kuwasilisha ritani na kulipa kodi stahiki kwa wakati.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako