• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya: Wanasiasa wataka viwanda vijengwe katika shamba la Del Monte

  (GMT+08:00) 2020-08-10 17:48:29

  WABUNGE watano kutoka Kaunti za Murang'a na Kiambu sasa wanaitaka serikali ihakikishe imezindua mradi wa viwanda katika shamba linalotarajiwa kutengwa kutoka miliki ya kampuni ya Marekani iliyoko Mjini Thika, Del Monte.

  Mradi huo walisema unafaa uwe na muundo wa Export Processing Zone (EPZ) ulio na uwezo wa kutoa nafasi zisizopungua 10, 000 za ajira kwa wenyeji.

  Kampuni hiyo ya utengenezaji juisi hasa za mananasi humiliki takriban ekari 22, 000 na ambazo kwa sasa zinazozaniwa na wenyeji wa Kaunti hizo mbili kutengwe angalau asilimia 30 yazo kuwafaa. Mzozo huo wa umiliki umesababisha kuzuka kwa kizungumkuti kuhusu kutolewa kwa hatimiliki ya kuendeleza mkataba wa Del Monte na Serikali ya Kenya kuhusu shamba hilo.

  Viongozi hao wanasema kuwa usoroveya unafaa kutekelezwa mara moja na ekari kamili zinazofaa kuwa katika umiliki wa Del Monte zibainike na hatimaye hatimiliki itolewe.

  Hata hivyo, waliisifia sana kampuni hiyo ya Del Monte. Walisema kuwa katika hali ngumu ya sasa kutokana na janga la Covid-19, kampuni hiyo haijafuta watu kazi wala kuwapunguzia mishahara.

  Wabunge hao walisema kuwa Kenya iko na jukumu la kulinda makampuni ya kigeni ambayo yamedhihirisha kuwa na uwezo wa kuinua hali ya maisha ya Wakenya ambao hasa hawana taaluma za kuwapa guu mbele katika soko la ajira.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako