• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya: Kenya kutumia Eliud Kipchoge kufufua utalii nchini

  (GMT+08:00) 2020-08-10 17:50:29

  Punde tu baada ya Kenya kukumbwa na jangala virusi vya corona, sekta ya Utalii ni mojawapo ya sekta zilizoathirika pakubwa sana. Sekta hiyo imepoteza mabilioni ya pesa na sasa serikali ya Kenya iko mbioni kuifufua.

  Bodi ya Utalii nchini Kenya imemteua mwanariadha tajika duniani Eliud Kipchoge kuwa balozi wa utalii wa kenya kwa dunia nzima. Kenyainatarajia kutumia umaarufu wa Kipchoge kuraia watalii wa Kenya na wale wa kigeni kuja kutalii Kenya.

  Eliud Kipchoge ambaye yuko katika mbuga ya kitaifa ya Maasai Mara na familia yake, aliwaraia wakenya kujitokeza na kutalii mbuga na vivutio vingine vya kitalii nchini Kenya.

  Rais Uhuru Kenya ambaye alizungumza na Kipchoge pamoja na waziri wa utalii Najib Balala kwa kutumia video, aliwarai wakenya kutumia fursa hii ambapo ada za utalii zimepunguzwa. Aidha rais alitoa ujumbe maalum kwa watalii wa kigeni kwamba wawe huru kuja nchini Kenya kutalii na wasiwe na wasiwasi wowote.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako