• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Raia 121 wa Ethiopia wakamatwa kwa tuhuma za kuhusika na shambulizi

    (GMT+08:00) 2020-08-11 09:50:07
    Ofisi ya Mawasiliano ya mkoa wa Benishangul Gumuz nchini Ethiopia imesema, imewashikilia watu 121 wanaotuhumiwa kuhusika na shambulizi lililotokea hivi karibuni lililosababisha vifo vya watu 13.

    Mwezi Julai, watu wasiojulikana waliwaua raia 13 na kuwajeruhi wengine kadhaa katika mkoa huo. Awali, maofisa nchini Ethiopia walisema shambulizi hilo lilikuwa na lengo la kikabila kwa kuwa watu waliouawa walitokea kabila la Amhara, ambao wamekaa kwenye eneo hilo kwa miongo kadhaa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako