• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Willian Borges da Silva apeana mkono wa kwaheri na Chelsea

    (GMT+08:00) 2020-08-11 18:10:28

    Kiungo mshambuliaji mzawa wa Brazil, Willian Borges da Silva, 32, amethibitisha kuondoka kambini mwa Chelsea baada ya kuwahudumia kwa kipindi cha miaka saba. Nyota huyo alikosa kuchezea Chelsea dhidi ya Arsenal katika fainali ya Kombe la FA mnamo Agosti 1, 2020, uwanjani Wembley, Uingereza na akawa nje ya kikosi kilichobanduliwa na Bayern Munich kwenye Klabu Bingwa Ulaya (UEFA) mnamo Agosti 8, 2020, kwa sababu ya jeraha la kifundo cha mguu. Kuagana kwake na Chelsea kunachangiwa na kukosekana kwa mwafaka kati yake na usimamizi uliokataa kurefusha mkataba wake kwa miaka mitatu zaidi ugani Stamford Bridge. Willian kwa sasa anasubiri kuingia katika usajili rasmi wa Arsenal wanaonolewa na kocha Mikel Arteta. Willian ameongoza Chelsea kunyanyua mataji matano, mawili yakiwa ya Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) na Europa League. Aliwahi kutawazwa mchezaji bora wa mwaka kambini mwa Chelsea mara mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako