• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya Benki ya Dunia yapiga jeki mpango wa Kazi Mtaani kwa Sh16.2 bilioni

  (GMT+08:00) 2020-08-11 19:39:34

  BENKI ya Dunia imepiga jeki mpango wa Kazi Mtaani nchini Kenya kwa kupatia serikali mkopo wa Sh16.2 bilioni kuimarisha huduma katika mitaa ya mabanda.

  Taarifa kutoka kwa benki hiyo imesema kwamba pesa hizo zitasaidia kuimarisha usalama wa wamiliki wa nyumba katika mitaa ya mabanda nchini Kenya kwa kuwapa hatimiliki, kuimarisha barabara, mitaro ya majitaka, maji usafi, taa za barabarani na vyoo pamoja na kusaidia wakazi kukabiliana na hatari zinazowakabili likiwemo janga la corona.

  Benki ya Dunia imejitolea kuendelea kuunga juhudi za serikali za mpango unaoendelea wa Kazi Mitaani katika awamu zijazo hadi ufaidi vijana 200,000 katika kaunti zote 47.

  kazi ya kuimarisha barabara itatoa ajira kwa wakazi wa mitaa ya mabanda walioathiriwa na janga la corona.

  Benki hiyo imesema pesa hizo zitafaidi wakazi 1.7 milioni wa mitaa ya mabanda iliyochaguliwa katika miji ya Kenya.

  Serikali ya Kenya ilianzisha mpango wa Kazi Mtaani ili kuwakinga vijana katika mitaa ya mabanda dhidi ya athari za kiuchumi kufuatia janga la corona. Rais Uhuru Kenyatta amesema serikali imetenga Sh10 bilioni kufanikisha mradi huo hadi Desemba mwaka huu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako