• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Sudan Baraza Kuu la Utawala wa Sudan na Baraza la Waziri limeidhinisha Mabadiliko katika bajeti ya 2020

  (GMT+08:00) 2020-08-11 19:40:40

  Baraza Kuu la Utawala wa Sudan na Baraza la Waziri limeidhinisha bajeti ya 2020 kupitiwa tena.

  Waziri wa Habari Feisal Mohamed Saleh amesema kuwa janga la corona limesababisha kupungua kwa mapato ya Taifa kwa asilimia 40, na kuongezeka kwa kiwango cha matumizi ya Taifa.

  Mabadiliko katika bajeti ya 2020 yalikuwa muhimu kupunguza athari mbaya ya kuenea kwa corona na athiri uchumi.

  Serikali iliidhinisha marekebisho ya polepole ya viwango vya kubadilishana vya Dola na kiwango cha forodha cha Dola kwa kipindi cha miaka mbili hadi bei halisi imefikiwa.

  Inatarajiwa kwamba uchumi utaanza kukua ifikapo mwisho wa 2021, ambayo ingechangia kupunguza mfumko mkubwa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako