• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatoa msaada kwa jamii ya Waislam nchini Sierra Leone kukabiliana na COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-08-12 09:49:20
    Ubalozi wa China nchini Sierra Leone jana umetoa msaada kwa jamii ya Waislam ili kuwasaidia kukabiliana na changamoto zilizosababishwa na janga la COVID-19. Msaada huo ni pamoja na barakoa 10, 000, tani 10 za mchele, ndoo 100 ya mafuta ya kupikia, na vipimajoto 10. Balozi wa China nchini humo Hu Zhangliang amesema, msaada huo utaimarisha zaidi uhusiano kati ya China na Sierra Leone, na kuahidi kuwa China itaendelea kuwaunga mkono watu wa Sierra Leone katika pande zote za uhusiano wa kidiplomasia na ushirikiano kati ya watu. Waziri wa Ustawi wa Jamii wa Sierra Leone Baindu Dassama amesema msaada huo unaonesha uhusiano wa kirafiki kati ya nchi hizo mbili, na atahakikisha vitu hivyo vinafikishwa kwa watu waliolengwa.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako