• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkuu wa ECA apongeza ushirikiano wa China na Afrika katika kukabiliana na janga la COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-08-12 09:50:58

    Mkurugenzi Mkuu wa Kamati ya Uchumi wa Afrika ya Umoja wa Mataifa (ECA) Bi. Vera Songwe amepongeza misaasa inayotolewa na China kwa Afrika katika kupambana na virusi vya Corona, na kutoa wito wa kuimarisha zaidi ushirikiano kati ya pande hizo mbili dhidi ya janga hilo.

    Bi. Songwe amesema hayo alipohojiwa na Shirika la Habari la China Xinhua mjini Addis Ababa, Ethiopia. Amesema, kuna uratibu mkubwa unaoendelea kati ya China na Afrika katika utafiti wa masuala ya kiafya ambao pia una umuhimu mkubwa.

    Pia ameipongeza China kwa kuiunga mkono Afrika katika kupambana na janga hilo, na kusisitiza umuhimu wa kuimarisha zaidi uhusiano wa pande hizo mbili ili kuziwezesha nchi za Afrika kuwa na fedha za kutosha kudhibiti mgogoro unaotokana na virusi vya Corona.

    Takwimu mpya zilizotolewa na Kituo cha Kukinga na Kudhibiti Magonjwa cha Afrika zinaonyesha kuwa, mpaka kufikia jana, idadi ya kesi zilizothibitishwa kuwa na virusi vya Corona barani Afrika iliongezeka na kufikia 1,055,964.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako