• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya: Benki ya Equity yanunua ile ya Banque Commerciale Du Congo

  (GMT+08:00) 2020-08-12 17:43:22

  Benki ya Equity ya Kenya imekamilisha ununuzi wa hisa nyingi katika benki ya DR Congo Banque Commerciale Du Congo (BCDC).

  Ununuzi huo ni wa kima cha dola milioni 95.

  Mnamo Septemba mwaka jana, Equity ilitangaza kuwa ilikubaliana na mmiliki wa hisa nyingi kwenye benki hiyo George Arthur Forrest kununua mgao wake wote kwa dola milioni 105.

  Hata hivyo George Arthur amepunguza bei kwa dola milioni 10.

  BCDC ilikuwa inamilikiwa kwa asilimia 66 na George Arthur Forrest na familia yake serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo asilimia 25 na asilimia nyingine 7 ikiwa ni wafanyabiashara wadogowadogo.

  Benki ya Equity, ikiwa na wateja zaidi ya milioni 14, ina matawi kote nchini Kenya, Uganda, Rwanda, Tanzania, Sudani Kusini, na DRC.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako