• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Viwanda na biashara Zanzibar vyapihga hatua, asema Rais

  (GMT+08:00) 2020-08-12 17:43:39

  Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein, amesema serikali imepata mafanikio makubwa katika kuendeleza na kuimarisha sekta za viwanda na biashara Zanzibar.

  Aliyasema hayo jana Ikulu mjini Zanzibar alipokutana na uongozi wa Wizara ya Biashara na Viwanda ilipowasilisha utekelezaji wa Mpango Kazi wa Mwaka 2019/20, na Mpango Kazi wa mwaka 2020/21.

  Dk. Shein alisema katika kipindi cha awamu ya saba ya uongozi wake, juhudi kubwa zimefanywa katika kuimarisha sheria, sera na miongozo mbalimbali na kuimarisha miundombinu muhimu kwa ukuaji wa sekta ya biashara na viwanda.

  Alisema misingi hiyo iliyojengwa ni vyema ikaendelezwa ili serikali ijayo ya awamu ya nane ianze utekelezaji wa mipango yake kwa kasi zaidi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako