• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Wajasiriamali walemavu mbeya wanufaika na milioni 70

    (GMT+08:00) 2020-08-12 17:44:32

    Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali, mkoani Mbeya, imetoa Sh. milioni 70 zinazotokana na asilimia 10 ya mapato ya ndani kwa kikundi cha wajasiriamali wenye ulemavu wilayani humo (Uwalemba) kwa ajili ya kukuza shughuli zao.

    Mkuu wa Wilaya ya Mbarali, Reuben Mfune, amesema kuwa fedha hizo ni utekelezaji wa sheria ya uwezeshaji wa makundi maalumu.

    Alisema kwa mujibu wa sheria asilimia 10 ya mapato ya ndani ya kila halmashauri inatakiwa kukopeshwa kwa vikundi vya wajasiriamali wa makundi matatu ambayo ni asilimia nne wanawake, nne vijana na mbili watu wenye ulemavu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako