• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Kiwanda cha ngozi kujengwa Dodoma

    (GMT+08:00) 2020-08-12 17:44:55

    Serikali imewataka wadau wa ngozi nchini kuchangamkia fursa ya uwapo wa kiwanda cha kuchakata ngozi kinachojengwa jijini Dodoma kuzalisha bidhaa mbalimbali zitokanazo na ngozi.

    Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhandisi Stella Manyanya kukagua kiwanda cha ngozi mjini Dodoma alisema kuwa mradi huo ukikamilika eneo hilo litakuwa kijiji cha ngozi hivyo ni wakati sahihi wa wadau wa ngozi kujitathimini na kuhakikisha ngozi zinafikishwa kwenye kiwanda hicho ili kutengeneza bidhaa zitokanazo na ngozi.

    Manyanya alisema kuwa ngozi itapatikana kutoka katika maeneo mengine hapa nchini.

    Aliagiza kiwanda hicho kujengwa kwa ubora unaohitajika , kusimamiwa vizuri ili kupata jengo bora, na matumizi ya fedha yaendane na ubora wa jengo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako