• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Idadi ya vifo kutokana na mapigano nchini Sudan Kusini yafikia 127

    (GMT+08:00) 2020-08-13 09:37:36

    Jeshi la serikali ya Sudan Kusini limethibitisha kuwa watu 127 wameuawa katika mapigano ya hivi karibuni kati ya jeshi hilo na raia katika eneo la Tonj, kaskazini mwa mkoa wa Warrap nchini humo.

    Msemaji wa jeshi hilo Lul Ruai Koang amesema, raia 82 na askari 45 wameuawa katika mapigano hayo yaliyoanza jumamosi iliyopita kufuatia kutoelewana kati ya askari hao na vijana katika soko moja lililoko eneo hilo.

    Habari nyingine zinasema, shirika la kibinadamu la Umoja wa Mataifa limelaani vikali mashambulizi ya kikatili dhidi ya wafanyakazi wa misaada ya kibinadamu katika eneo la Central Equatoria, nchini Sudan Kusini.

    Msafara wa Shirika la Kimataifa ulishambuliwa na kundi la watu waliokuwa na silaha huko Abegi katika barabara ya Yei-Lasu karibu na mji wa Yei siku ya jumatatu. Wafanyakazi wa Shirika hilo ambalo ni mwenza wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) walikuwa njiani kuelekea kwenye kambi ya Lasu inayowahifadhi wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Sudan kutoa huduma za afya, lishe, na usafi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako