• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wasafiri kununua tiketi za usafiri wa boti za Azam kwa njia ya simu

    (GMT+08:00) 2020-08-13 19:24:05

    Wateja wa mtandao wa simu wa Zantel nchini Tanzania watanunua tiketi za usafiri wa boti za Azam kwa njia ya Ezypesa baada ya kampuni hiyo kuingia ubia na kampuni ya usafirishaji ya Kilimanjaro Fast Ferries Ltd inayotoa huduma za usafiri wa boti.

    Kampuni hiyo ni moja ya watoa huduma za usafiri wa majini kati ya Zanzibar na Dar es Salaam ikiwa na boti nne zinazochangia katika urahisishaji wa huduma za usafiri kwa wenyeji na wageni.

    Mkuu wa Masoko na Huduma za Kifedha wa Zantel, Sakyi Opoku. alisema hatua hiyo imelenga kurahisisha upatikanaji wa huduma za ukataji tiketi kwa abiria, hivyo kuboresha maisha ya wateja wao.

    Opoku alisema wanaamini njia hiyo ni suluhisho na itaboresha namna wateja wanavyopata huduma za usafiri hususan wasafiri wa ndani kwani kwa sasa hakuna haja ya kwenda tena katika ofisi bali ukiwa na simu yako tu unaweza kujihakikishia uhakika wa kupata usafiri.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako