• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wafanyabiashara wa mitumba wafanya maandamano nchini Kenya

  (GMT+08:00) 2020-08-13 19:24:24

  Wafanyabiashara wa nguo za mitumba nchini Kenya jana walifanya maandamano katika miji mbalimbali wakiishinikiza serikali iwaruhusu kuagiza bidhaa kutoka nchi za kigeni.

  Katika Kaunti ya Nairobi, maandamano yalifanywa katika soko la Gikomba.

  Wafanyabiashara hao wanasema serikali haijafafanua kuhusu ni lini watakubaliwa kuagiza bidhaa.

  Walisema wana madeni ya kulipa katika sehemu zao za biashara na pia mahitaji ya nyumbani.

  Wafanyabaisahara hao wanataka marufuku ya kutoagiza mitumba kutoka nchi za kigeni kuondolewa.

  Kupitia msemaji wao Bw Peter Njoroge, wafanyabiashara hao walisema wengi wao wamepoteza ajira katika sekta mbalimbali baada ya viwanda, mikahawa, sehemu za burudani na sekta ya utalii kukosa wateja.

  Waziri wa Biashara, Bi Betty Maina alisema bado kuna vikwazo kuhusu uagizaji wa bidhaa nyingi kutoka nchi za kigeni.

  Aidha Bi Maina alisema Wizara ya afya inafaa kutoa mwelekeo kuhusu jinsi ambavyo uagizaji wa mitumba unapaswa kufanywa na pia kutoa ushauri kuhusiana na athari zake.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako