• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati Zanzibar kutoa leseni kwa wasambazaji gesi

    (GMT+08:00) 2020-08-13 19:24:50

    Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati Zanzibar (ZURA), inatarajia kutoa leseni kwa wauzaji na wasambazaji wakubwa wa gesi nchini ili kuhakikisha biashara hiyo inaendeshwa kwa misingi ya usalama.

    Akizungumza jana na waandishi wa habari, Ofisa Uhusiano wa mamlaka hiyo, Hassan Juma Amour, alisema kuwa hadi sasa mamlaka hiyo imeshapokea maombi ya wafanyabiashara watano wanaoingiza bidhaa hiyo nchini humo na wasambaji tisa kwa ajili ya kupatiwa leseni.

    Alisema, hatua hiyo imefikiwa baada ya mamlaka hiyo kuridhishwa na hatua ya utoaji wa elimu juu ya kanuni ya gesi ya kupikia (LPG) ya mwaka 2017 na miongozo ya gesi kwa ajili ya kusimamia uendeshaji wa biashara hiyo Zanzibar.

    Alisema lengo la mamlaka hiyo kutoa leseni hizo ni kuweka usimamizi madhubuti wa biashara hiyo na kujua muingizaji na muuzaji wa rejareja anaendesha vipi biashara hiyo na kama anasimamia misingi ya usalama na viwango vinavyokubalika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako