• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wauzaji Bidhaa Za Wanafunzi Walalama Kenya

  (GMT+08:00) 2020-08-14 18:52:25

  Wafanya biashara wanaojihusisha na bidhaa za shule nchini Kenya wamelalamikia hatua ya kufungwa kwa shule hadi mwaka 2021 kuwa ni pigo kubwa kwa biashara zao. Wamesema hali zao za kifedha zinaendelea kuzorota tangu kufungwa kwa shule zote nchini humo Machi 15 kufuatia kuzuka kwa ugonjwa wa Covid-19.

  Walisema wanahofia kuzama katika dimbwi la umaskini kwani wanalazimika kutumia akiba kulipa ada mbalimbali zikiwemo kodi ya duka na ada za leseni licha ya biashara zao kuwa haziwaingizii kipato chochote.

  Kulingana na Waziri wa Elimu Bw George Magoha shule hazitafunguliwa mwezi Septemba kama walivyokuwa wamepanga awali kufuatia kuongezeka kwa idadi ya maambukizi ya ugonjwa huo nchini.

  Aidha walisema baadhi yao wameanza kufunga biashara kwa kushindwa na gharama za kuendesha biashara hizo.

  Bw Magoha aliagiza shule zifunguliwa Januari 2021 ikiwa idadi ya visa vya maambukizi itakuwa imeteremka pakubwa akisema kuwa kufunguliwa kwa shule hizo kwa sasa kutahatarisha afya za wanafunzi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako