• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganga yazindua mpango wa kuunda ajira na kuongeza mapato ya watu nchini humo

    (GMT+08:00) 2020-08-14 18:53:06

    Serikali ya Uganda imezindua mpango wa rais wa kuunda ajira na utajiri katika wilaya ya Kabarole ukiwa na lengo la kuimarisha mapato ya watu nchini humo. Akizindua mpango huo, mkuu wa ofisi inayosimamia mpango huo wa rais Bi Ritah Namuwenge amesema mpango huo ambao ni mpya unatazamiwa kuunda ajira nyingi na pia kuimarisha mapato ya watu wa kawaida. Ameongeza kuwa imekuwa ni vigumu kwa watu wengi nchini Uganda kufikia huduma za fedha lakini mpango huo wa serikali utarahisisha utaratibu wa kila mmoja kufikia huduma za fedha nchini humo. Mpango huo wa serikali utawafanya pia watu wengi nchini Uganda kutumia vyema huduma za fedha ili kujijenga kiuchumi. Mpango huo unakuja wakati ambapo idadi ya watu masikini inazidi kuongezeka nchini Uganda hasa wakati huu ambapo janga la Corona limeendelea kuwaathiri wafanya biashara wengi nchini humo na pia kusababisha watu wengi kuachishwa kazi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako