• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watanzania wapongezwa kwa changamkia bidhaa za ndani

    (GMT+08:00) 2020-08-14 18:53:25

    Raia watanzania wamepongezwa kwa kuchangamkia bidhaa zinazotengenezwa nchini humo tofauti na awali. Katibu mkuu mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) nchini Tanzania Bw Beng'i Issa amesema awali Watanzania walikuwa wakithamini zaidi bidhaa kutoka nje kuliko zinazozalishwa ndani lakini kutokana na ongezeko la viwanda nchini humo na ubora wa bidhaa, vimesababisha kubadili mtazamo .

    Ameongeza kuwa baraza hilo linathamini wajasiriamali wadogo na kushirikiana nao ili kuwainua na kuwa wafanyabiashara wakubwa.

    Aidha Issa aliwaahidibaadhi ya wajasiriamali mikopo ili kupiga jeki biashara zao. Aidha amesema kuwa kwa sasa vibali vingi vinapatikana bila kuwepo kwa urasimu kwenye taasisi husika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako