• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya: Serikali yaondoa marufuku ya uagizaji wa nguo za mitumba Read

  (GMT+08:00) 2020-08-17 16:53:38
  Serikali imelegeza marufuku ya uagizaji wa nguo zilizotumika almaarufu mitumba na sasa wafanyabiashara wa bidhaa hiyo wanaweza kurejelea biashara yao. Shirika la Ukadiriaji Ubora wa Bidhaa(KEBS) pamoja na Wizara ya Biashara, zilichapisha sheria mpya ambazo zinatazamiwa kufuatwa na wafanyabiashara pamoja na wanunuzi.

  Katika kanuni hizo mpya, kifurushi kimoja cha bidhaa hiyo kinatakiwa kuwa na aina moja ya nguo na kuchapishwa uzani wake, jina la muuzaji, taifa ambalo lilitokea na anwani ya muagizaji. Hata hivyo, kutakuwa na vikwazo katika kuagiza nguo kama vile za kulala, nguo za ndani na taulo. Mzigo wa viatu pia utakuwa wa aina moja na pia utapachikwa uzani wake, na anwani za muagizaji na muuzaji.

  Wale ambao wanaendesha maduka ya kuuza nguo za mitumba wanatarajiwa kufuata masharti ya COVID-19 yaliyowekwa na Wizara ya Afya ikiwemo kunyunyuzia maduka yao dawa, kuweka vituo vya kunawa mikono na kuvalia maski. Wale wauzaji reje reja watalazimika kutafuta leseni ili kuendelea na biashara yao na kufuata masharti ya kuzuia kusambaa kwa virusi hivyo.

  Wanunuzi wamehimizwa kununua mitumba kutoka kwa wauzaji walioidhinishwa pekee. Serikali ilipiga marufuku uagizaji wa nguo za mitumba mapema mwaka huu kama mojawapo ya njia za kuzuia kusambaa kwa COVID-19

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako