• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • DRC: Mgomo wasitishwa katika sekta ya mafuta kusini na mashariki mwa DRC.

    (GMT+08:00) 2020-08-17 16:54:08
    Wafanyabiashara katika sekta ya mafuta katika ukanda wa kusini na mashariki mwa DRC wamesitisha mgomo wao uliokuwepo wiki jana, baada ya mazungumzo na waziri mkuu wa nchi hiyo.

    Serkali ya Kinshasa imetoa jibu kwa madai yao. Kwa sasa bei ya lita moja ya mafuta aina ya petroli imepanda kwa kiwango cha 24%, jambo ambalo si rahisi kwa wanunuzi.

    Mazungumzo kati ya Waziri Mkuu Sylvestre Ilunga Ilukamba na ujumbe wa wafanyabiashara katika sekta ya mafuta yalidumu siku mbili jijini Kinshasa.

    Pande zote mbili zimefikia makubaliano hasa kuhusu bei ya petroli. Sasa lita moja ya mafuta itauzwa senti 93 badala ya 75, bei iliyokuwa ikiuzwa hapoa awali. Bei imependa kwa kiwango cha 24%.

    Albert Yuma, kiongozi wa muungano wa vyama vya wafanyibiashara alitoa wito kwa wafanyibiashara kuwa mgomo hautawafaidi na chochote, bali kusababisha uchumi kudidimia. Bei ya lita moja ya petroli mitaani ilikuwa ikiuzwa dola 2 za kimarekani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako