• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Sekta ya kilimo yakua kwa asilimia tano.

    (GMT+08:00) 2020-08-17 16:54:30
    Sekta ya kilimo nchini Tanzania imeelezwa kuendelea kukua kwa wastani wa asilimia 5.2, huku sekta ndogo ya mazao ikikuka kwa asilimia 5.8 na kuchangia ongezeko la kasi ya ukuaji wa uchumi.

    Haya yalibainishwa mwishoni mwa wiki jana na Kamishna wa Uendelezaji Sekta ya Fedha nchini humo,Charles Mwamaja. Kwa mujibu wa Mwamaja, pato la taifa linalotokana na kilimo kwa kutumia bei za mwaka wa 2015, limeongezeka kwa asilimia 17 kutoka shilingi trilioni 25.2 mwaka wa 2015 hadi shilingi trilioni 29 kwa mwaka jana. Alisema hali hiyo inaonyesha jinsi sekta hiyo inavyoendelea kukua.

    Mwaka wa 2018, sekta ya kilimo ilichangia asilimia 28.2 ya pato la taifa. Kati ya mwaka wa 2015 na 2019, seka ya kilimo imeendelea kukua kwa wastani wa asilimia 5.2.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako