• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Timu ya Yanga yaendelea kuimarisha kikosi chake kwa ajili ya ligi kuu

    (GMT+08:00) 2020-08-18 19:07:27

    Siku chache baada ya Simba kuonesha makali katika kuimarisha kikosi chake, klabu ya Yanga nayo imeamua kufuata mwelekeo huo kwa kutangaza wachezaji wake wapya iliowasajili. Yanga ambayo imejikita zaidi kufanya usajili wa ndani, tayari imemnasa kijana Zawadi Mauya (27), ambaye ameahidi kufanya juhudi kuonesha uwezo wako, lakini ni wazi kuwa atakumbana na changamoto ya kupata nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza kutoka kwa Feisal Salum na Abdulaziz Makame na kukiri alishawasoma tangu akiwa Kagera Sugar. Mauya ni kati ya wachezaji saba waliosajiliwa ndani ya kikosi hicho, wengine ni Waziri Junior (Mbao FC), Bakari Mwamnyeto (Coastal Union), Kibwana Shomary (Mtibwa Sugar), Mustapha Yassin (Polisi Tanzania), Farid Mussa (CD Tenerife B) na Abdallah Shaibu 'Ninja' (MFK ya Jamhuri ya Czech). Kijana Zawadi Mauya amezungumzia mambo mengi kuhusu soka lake ikiwamo jambo moja la kusikitisha linalohusu mauaji ya mwenzake aliyechomwa kisu hadi kufa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako