• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Barcelona wamtimua kocha baada ya kipigo kikali kutoka kwa Bayern Munich

    (GMT+08:00) 2020-08-18 19:07:45

    Klabu ya Barcelona ya Hispania inapanga kumtangaza Ronald Koeman kuwa kocha wake mpya baada ya Quique Setién kufukuzwa kazi Jumatatu jioni, akiwa amedumu miezi sita tu kwenye kazi hiyo. Bodi ya wakurugenzi imekubaliana kwamba Quique Setién sio kocha tena wa timu ya kwanza, na uamuzi huu unatokana na marekebisho mapana ya timu ya kwanza. Ronald Koeman kwa sasa ni kocha wa timu ya taifa ya Uholanzi, anatarajiwa kuiweka pembeni timu hiyo na kuanza kazi Barca baada ya wiki hii. Uamuzi ulifikiwa kumeleta Mholanzi huyo baada ya mkutano wa bodi uliofanyika kwa muda wa saa tatu huko Camp Nou Jumatatu, kabla ya kuondoka kwa Setién. Koeman mwenye umri wa miaka 57 amesema sio siri kuwa anatamani kuwa mwalimu wa Barcelona, na anapenda kuondoa aibu kama ile ya kufedheheshwa kwa kufungwa magoli 8-2 na Bayern Munich. Mwanzoni kulikuwa na majina mengine yaliyotajwa kuhusishwa na nafasi ya ukocha Barca, ikiwa ni pamoja na Thierry Henry, Xavi na Pochettino.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako