• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kipigo cha magoli 8-2 chamfanya Messi afikirie kuondoka Hispania.

    (GMT+08:00) 2020-08-18 19:08:06

    Lionel Messi ametangaza kutaka kuondoka Barcelona msimu huu, kwa mujibu wa taarifa zilizopo nchini Hispania. Nyota huyo wa kimataifa wa Argentina amedaiwa kutaka kuondoka katika klabu hiyo ya Hispania na inasemekana ameshawaambia mabosi. Messi alikasirika baada ya Barca kudhalilishwa kwa kipigo cha mabao 8-2 na kutolewa katika hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya Ijumaa iliyopita na Bayern Munich. Iliripotiwa kuwa mshambuliaji huyo alitishia kugoma kusaini mkataba mpya kama hakutakuwa na usajili wa kueleweka utakaofanywa na miamba hao wa Nou Camp. Lakini pia anaonekana kama si mtu wa kusubiri mabadiliko hayo ya wachezaji wapya na badala yake anahitaji kuondoka haraka iwezekanavyo. Lakini Barcelona yenyewe ilikanusha kuwepo kwa taarifa hizo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako