• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mwanasoka wa Kenya apoteza maisha baada ya kujeruhiwa kwenye mechi ya kirafiki

    (GMT+08:00) 2020-08-19 16:55:11

    Kocha wa klabu ya Shabana FC Vincent Nyaberi ametaja kifo cha mlinzi wa klabu hiyo Evans Obutu kama "pigo makubwa" kwa juhudi za timu hiyo kupata nafasi ya kucheza ligi kuu ya Kenya (KPL) msimu ujao. Mlinzi huyo, Evans Obutu mwenye umri wa miaka 33, ambaye alikuwa Shabana kwa mkopo kutoka Posta Ranger, alilazwa na jeraha la tumbo ambalo alipata Ijumaa wakati wa mchezo wa kirafiki kati ya timu zisizo za ligi, Town Warriors na Patarion kwenye uwanja wa Shule ya Msingi ya Gesure katika Kaunti ya Nyamira. Mechi hiyo ilisimamishwa katika dakika ya 40 baada ya mchezaji huyo kugongana na golikipa. Baadaye alikimbizwa katika Hospitali ya Rufaa ya Kisii (KTRH) lakini hakuhudumiwa kutokana na kuwa wahudumu wa afya walikuwa kwenye mgomo. Alipelekwa kwenye hospitali ya Nyangena, ambako baada ya matibabu alipoteza maisha yake.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako