• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya: Faida ya nusu mwaka ya benki ya Equity yapungua kwa asilimia 24

  (GMT+08:00) 2020-08-19 17:07:22

  Faida ya nusu mwaka ya benki ya Equity nchini Kenya imepungua kwa asilimia 24.3 hadi Shilingi bilioni 9.02.

  Upungufu huo ni kutoka Shilingi bilioni 11.92 kipindi kama hicho mwaka jana, na kuifanya Equity kuwa benki ya nne kushindwa kukuza mapato katika mazingira ya Covid-19.

  Faida ya jumla ya ilishuka kwa asilimia 26 hadi Shilingi bilioni 7.2 ikiwa ni asilimia 80 ya mapato yote ya benki hiyo.

  Upungfufu huo wa faida umeshuhudiwa licha ya mapato ya jumla ya riba kuongezeka kwa asilimia 16.9 hadi Shilingi 24.6 nayo mikopo ikiongezeka kwa shilingi bilioni 70.7 bilioni.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako