• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Uganda: Shilingi ya Uganda yasalia imara dhidi ya dola

  (GMT+08:00) 2020-08-19 17:07:41

  Benki kuu ya Uganda inasema shilingi ya nchi hiyo imendela kusalia imara dhidi ya dola kutokana na kupungua kwa uagizaji bidhaa kutoka nje.

  Shilingi imesalia thabiti huku kukiwa na athari mbaya zilizoletwa na Covid-19.

  Kulingana na wachambuzi, shilingi pia imesaidiwa na fedha za kigeni kutoka kwa mashirika yasiyokuwa ya kiserikali na misaada inaohusiana na Covid-19 kutoka kwa jamii ya kimataifa.

  Tangu mwezi Juni, shilingi iliongezeka dhidi ya dola kwa karibu asilimia 1.4, haswa kutokana na mahitaji ya chini kutoka kwa waagizaji na wazalishaji.

  Hata hivyo, shilingi ya Uganda imekuwa dhaifu dhidi ya Euro na Paundi ikipungua kwa asilimia 1.8 na asilimia 0.4, mtawaliwa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako