• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya: Kenya yapanga kuanza mradi mkubwa wa kawi ya nyuklia

  (GMT+08:00) 2020-08-19 17:08:05

  Kenya inapanga kujenga kiwanda cha nguvu ya nyuklia cha dola bilioni 5 (Sh540 bilioni) katika kaunti ya Tana River katika kipindi cha miaka saba ijayo kwafadhili kutoka kwa wawekezaji binafsi.

  Bodi ya Umeme wa Nyuklia ya Kenya (KNEB) imesema kwamba kiwanda hicho chenye uwezo wa awali wa kuzalisha megawati 1,000 kitajengwa na kuendeshwa na wawekezaji wa kibinafsi.

  Serikali inapanga kuongeza mara nne uzalishaji huo ifikapo mwaka wa 2035 chini ya mpango wa kujenga, kuendesha na kuhamisha (BOT).

  Kenya inachukulia nguvu ya nyuklia kama suluhisho la muda mrefu la gharama kubwa za mafuta na njia madhubuti ya kukata uzalishaji wa kaboni kutoka kwa sekta inayozalisha kawi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako