• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda: Mapato ya sukari yapungua Uganda

    (GMT+08:00) 2020-08-19 17:08:25

    Mapato ya sukari ya Uganda inayouzwa nje yamepungua kwa asilimia 54 kufuatia kufungwa kwa masoko katika nchi jirani.

    Kulingana na Benki ya Uganda, hadi mwezi Juni mapato ya mauzo ya nje ya sukari yalipungua hadi dola milioni 7.4m kutoka dola milioni 11.4 za mwezi Mei.

    Katika kipindi hicho, Uganda iliuza nje jumla ya tani 14,991 kutoka tani 23,212 mwezi Mei.

    Wataalam wa Viwanda wamesema uuzaji nje wa bidhaa hiyo unaweza kupungua zaidi ikiwa mizozo na nchi jirani, ambazo ni waagizaji muhimu haitatatuliwa.

    Mwezi uliopita Kenya ilifuta vibali vyote vya wauzaji wa sukari kutoka Uganda, ikisema soko lake lilikuwa limejaa sukari ya bei rahisi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako