• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mpango wa kwanza wa Biashara ya Huria la Afrika kufanywa Januari 2021.

    (GMT+08:00) 2020-08-19 17:08:44

    Umoja wa Afrika umetangaza kwamba mpango wa kwanza wa kibiashara chini ya eneo la Biashara ya Huria la Afrika (AfCFTA) unatarajiwa kufanywa Januari 1, 2021.

    Mwezi Aprili, Katibu Mkuu wa AfCFTA Wamkele Mene alisema utekelezaji wa makubaliano ya biashara huru Afrika hautaweza kuanza Julai 1 kama ilivyopangwa kwa sababu ya janga la corona.

    Umoja wa mataifa unasema AfCFTA itatoa fursa kwa Afrika kuunda tena minyororo ya usambazaji, kupunguza utegemezi kwa wengine na kuharakisha uanzishaji wa minyororo ya thamani ya kikanda ambayo itakuza biashara ya ndani ya bara hilo.

    Ripoti ya Benki ya Dunia inasema utekelezaji wa AfCFTA utapunguza athari hasi za COVID-19 kwenye ukuaji wa uchumi kwa kuongeza biashara ya kikanda na kupunguza gharama za biashara.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako