• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tanzania: Wakulima 83,000 Tanzania kupata mbolea bila malipo

  (GMT+08:00) 2020-08-19 17:09:06

  Wakulima 83,000 nchini Tanzania watanufaika kwa kupata mbolea bila malipo kwa lengo la kuongeza uzalishaji wa mpunga na mahindi.

  Uwezeshaji huo utafanywa na kampuni ya mbolea ya YARA Tanzania, ambapo Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo, Winston Odhiambo, amesema zaidi ya tani 12,500 za mbolea ya YaraMila Cereal yenye thamani ya shilingi bilioni 16.5 zitagawiwa kwa wakulima wadogo.

  Odhiambo alisema chini ya mpango huo, mkulima atahitajikakujisajili kupitia namba *149*46*16# ambapo kitambulisho cha mpigakura na cha taifa kitatumika katika kukamilisha usajili sambamba na kuzawadiwa mbolea.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako